Rais Dkt. Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Burudani ya muziki wa Taarabu asilia.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alikuwa mgeni rasmi katika Burudani ya muziki wa Taarabu asilia, ilioandaliwa maalum kwa ajili ya maadhimisho ya kusherehekea miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil, Kikwajuni jijini Zanzibar, ambapo magwiji wa sanaa ya muziki